Jinsi Ya Kumfanya Msichana Unayemtongoza au Uliyenaye Kwenye Mwanzo wa Uhusiano Awe na Hisia na Akupende Kupitiliza.
Kweli unataka kumvutia huyo msichana spesho aliyeuteka moyo wako na kukufanya usile usilale kwa mawazo juu yake achanganyikiwe na kukuweka wewe akilini mwake endelea kusoma kiumeni.com tukuweke wazi ni nini na ni kipi ufanye uuteke moyo wa huyo mrembo kwa marefu na mapana, na awe anakuwaza wewe tu na kukufikiria wewe kokote anako kwenda.
Kiumeni.com, nyumbani kwa wanaume tunakupa njia za kufanya ambazo zinahitaji utulivu, subila na kuzielewa kwa kina ili uweze kufanikisha wakati wa kumtongoza au mwanzo wa mahusiano ili huyu mrembo akuweke moyoni na rohoni.
#1; Kuwa shujaa wake...
Wakati wote anapokuwa na shida, matatizo au amekumbwa na mawazo yanayomtinga na kumchanganya akili, hakikisha unakuwa naye pamoja, na si kwa kukaa pembeni yake tu bali kwa kuonyesha dhahiri umeguswa na upo nae bega kwa bega kutafuta utatuzi, ufafanuzi wa kumwondolea dhahama iliyopo mrangoni kwake, weka jambo moja kichwani na unisikie vizuri, sio kila jambo utaliweza kulitatua na hicho pia akimaanishi kwa kuwa jambo lipo nje ya uwezo wako ndo hautakuwa na msaada, hata ushauri na maneno ya kumpa moyo yanatosha kumfanya uwe shujaa katika dunia yake hasa katika wakati wa matatizo.
Muulize ni kwa jinsi gani unaweza kumsaidia ila usiwe king'ang'anizi wa kutoa msaada wakati bado moyo wake haujakubaliana na wewe katika msaada huo, usitumie razima, tumia maneno mazuri ambayo ataona upo kwa ajiri ya kumsaidia na si vinginevyo.
Kama tayari ameshaonyesha kupendezwa na wewe, nenda nje ya mipaka yako na fanya kitu ambacho kitamstaajabisha na kama bado hajaonyesha kupendezwa na wewe, tumia utaratibu, subira na upole na atajikuta kaingia kwenye kumi na nane mwenyewe, kama wahenga wasemavyo "maneno mazuri humtoa nyoka pangoni".
#2; Hakikisha asikuchukulie kama rafiki...
Fanya urafiki naye ila siyo kila saa unakaanaye karibu sana naye, heshima hushuka hasa mtu mkizoeana sana na kwa mwanamke hupoteza ile hali ya mvuto na hamasa na kuanza kukuona mtu wa kawaida, na iwapo akikuchukulia kama rafiki au kaka, kumrudishia tena hisia ili akuchukulie zaidi ya hapo huwa inakuwa ni ngumu.
Hakikisha kwa muda wote unapokuwa nae mwonyeshe kwa kumjari kuwa unahisia nae, na sio kwa kumwambia ila acha vitendo vyako vyenyewe vizungumze juu ya kile moyo wako unachojisikia na atakuona wewe ni mwanaume wa kipekee maana vitendo kwa mwanamke hukonga moyo zaidi tofauti na maneno hewa na ahadi zisizokwisha, na hii itampa urahisi mwanamke kujua ni kundi gani ndani ya moyo wake atakalokuweka, akuweke kihisia au kirafiki.
#3; Mpe muda wa kukuwazia upo wapi na unafanya nini...
Siyo kila saa ni saa ya kuongea naye au kuwa naye, ukisha muweka karibu na kunfanyia vitendo vya wazi ni kipi kilichomo moyoni mwako ni vizuri ukawa unampa muda wa kuwa naye mbali ili naye akufikirie, kuongeza mvuto na kujua uzito wako kwenye maisha yake kwa ujumla, afikirie vitendo vizuri unavyomfanyia, kwa jinsi atakavyokuwa anaendelea kukuwaza ndo jinsi ambavyo nawe unamwingia akilini na kuuteka moyo wake.
Najua unajua ila ningependa nikujulishe zaidi, kama wahenga wasemavyo "mtu akikuzoea sana, dharau huanza na anakua anakuchukulia kwa wepesi", kwa hio mazoea ni mabaya hasa mwanzo mwa uhusiano au kipindi cha utongozaji, na hapa kaka sijaongelea mazoea yale ya kawaida ya kumfanya aondoe uwoga juu yako, naongelea mazoea ya kupitiliza ya kumafata fata mwanamke kama kuku.
#4; Angalia na tilia mkazo unachovaa...
Marafiki wa kawaida hawawezi kujali iwapo umerudia nguo zile zile
ulizokuwa umezivaa tangia jana ila msichana wa ndoto zako huwezi
kumuingia akilini iwapo ukiwa katika hali ya uchafu na kutokuwa nadhifu,
kwa utafiti uliofanyika katika chuo kimoja jijini washingtoni marekani
cha saikolojia na tabia za binadamu , unadhifu huwavutia zaidi ndo maana
kisaikolojia wanawake
wanapokutana na mtu kwa mara ya kwanza humuangalia juu mpaka chini,
inawezekana ukajua wakati anakutathimini au usijue ila ni jambo ambalo
lazima mwanamke hulifanya, na kwa kufanya hivyo huweza kukutambua tabia zako
na jinsi unavyoishi na iwapo ukiongea nae, huweza pia kutambua tabia ya
hisia yako kama wewe ni mkali au mpole na tabia nyinginezo.
Kama kaka angu Abeli asemavyo, "uvaaji wa binadamu na jinsi anavyokaa
kimwili ni dirisha la roho yake, maana humuongelea yote na jinsi maisha
yake yalivyo".
Hakikisha unaoga na kuwa msafi na nadhifu, kama unandevu zinyoe ziwe
katika stairi na hali nzuri, nukia kuwa nadhifu na vaa nguo zinazoendana
na mwili wako, fanya mazoezi ya mara kwa mara kuufanya mwili wako kuwa
katika hali ya kiume na kishupavu na inayovutia zaidi.
#5; Kuwa mcheshi...
Kuwa na uelewa wa kiakili, jua nini cha kuzungumza kulingana na mazingira, jua mambo mbalimbali ya kijamii ili upate wigo mkubwa wa kuzungumzia na kamwe usionyeshe hata kidogo hali ya ujuwaji wa uwewe ndie wewe... kila kitu ndo unakijua.
#6; Kuwa mtu wa uhakika na kuaminika...
Wanawake hupenda mtu wa uhakika, tenda kutokana na kile ulichomuhaidi na kuongea na kama ulitoa ahadi, vitendo ulivyovihaidi vifanye katika muda uliopanga kuvifanya, usiwe mzungushaji wa mambo, na iwapo ukiahidi kufika sehemu hakikisha unalinda muda ulioupanga utafika, wanawake hawapendi kumsubilia mtu, wanahisi kama umeshindwa kumthamini na kumchukulia katika uzito unaotakiwa, kama vile unamchukulia juu juu na hivyo nafsi yake itabadilia na kuanza kukuchukulia na wewe juu juu.
Na katu usitumie utani kwenye mapenzi, utani utani uliovuka mpaka hukutoa katika ngazi ya juu ya moyo wake na kukuweka kama mtu wa kawaida, utani uondoa uhakika, ukimwambia kitu atakuwa anahisi unamtania.
Utani ndo nguzo kubwa itakayokufanya akutoe moyoni na kukuona kama rafiki.
Kuwa na sifa nzuri mtaani ili hata kama yeye au rafiki zake wakikufanyia uchunguzi wakuone wewe ni wa uhakika na siyo wakute sifa chafu ambazo zitakuondolea sifa nzuri unazoumia na kutumia nguvu kubwa kuzijenga, sifa kama ulimwacha mpenzi wako wa zamani kwa ajiri ya msichana mwingine ndo hasa zitakazokuondoa moyoni mwake na atakuchukulia kama muongo fulani ambae kwake hautafuti kingine bali kile kilichopo ndani ya chupi yake.
Jiheshimu na onyesha heshima kwa unavyompenda na sio kutumia maneno machafu ya aibu ya kihuni na hapo kwake moyoni utamuingia kwa sababu anauhakika na kukuamini wewe.
KUTAZAMA UGOMVI WA ALLY KIBA NA DIAMOND PLATNUMZ BONYEZA HAPA CHINI=>>>

Jinsi Ya Kumfanya Msichana Unayemtongoza au Uliyenaye Kwenye Mwanzo wa Uhusiano Awe na Hisia na Akupende Kupitiliza.
Reviewed by maajabu
on
March 04, 2018
Rating:
Reviewed by maajabu
on
March 04, 2018
Rating:

No comments: